Nlipomaliza kutoa maelezo juu ya kijitabu hiki chenye baraka na chenye manufaa nikaona kuwa katika kukamilisha manufaa yake ni kufuata mwenendo wa mwandishi wake (Rahimahu Allaah) katika kuchunguza kwa undani masuala ambayo majaribu yake ni mengi na maswali juu yake ni mengi na yana uhusiano wa karibu sana na mada yake, nayo ni:

1 – Kupaka juu ya viatu.

2 – Kupaka juu ya soksi ya ngozi au soksi iliyochanika.

3 – Je, wudhuu´ unachenguka kwa kuvua kilichopakwa juu yake?

4 – Ni lini unaanza muda wa kupaka?

5 – Je, wudhuu´ unachenguka kwa kuisha kwa muda wa kupaka?

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 81
  • Imechapishwa: 22/04/2026