01. Idhini ya Shaykh al-Fawzaan kuchapisha kitabu

Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, ambaye ndiye Mtume wa mwisho, kizazi chake, Maswahabah wake na wale watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.

Amma ba´d:

Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ

“Enyi walioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu na wala msifuate nyayo za shaytwaan; hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.” (02:208)

Huu ni ufafanuzi wa kitabu “Nawaaqidh-ul-Islaam” cha Shaykh-ul-Islaam Mujaddid Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) niliyoitoa Msikitini. Baadhi ya ndugu wakaonelea kuziandika kwa kuzitoa katika mkanda na kukichapisha na wakaniomba idhini kwa hilo ambapo nikawapa kwa kutarajia ndani yake kutakuwepo kitu katika faida. Aliyesimama kwa kazi hii ni Shaykh muheshimiwa ndugu Muhammad bin Fahd al-Haswiyn. Allaah amjaze kheri na anufaishe kupitia kwake. Nimempa idhini ya kukieneza na kukichapisha.

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah wake.

Imeandikwa na:

Swaalih bin Fawzaan bin ´Abdillaah al-Fawzaan

05-11-1424

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 05
  • Imechapishwa: 06/02/2017