Umbile la wanawake wa duniani Peponi

Swali: Je, mwanaume Peponi atakuwa na wake wengi? Ambaye yuko na wake wane duniani atakuwa nao ikiwa kama watakuwa ni waumini na waislamu?

Jibu: Wanawake wa duniani ambao ni waumini watafanywa kuwa wazuri uzuri usiokuwa na kifani. Allaah (Ta´ala) Amesema:

إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا عُرُبًا أَتْرَابًا لِّأَصْحَابِ الْيَمِينِ

“Hakika Sisi Tunawaanzisha [al-Huur al-´Aiyn] uanzishaji. Tunawafanya mabikra. Wenye mahaba kwa waume zao, hirimu moja. Kwa ajili ya watu wa kuliani.” (56:35-38)

Umbile la wanawake wa duniani ambao ni waumini litafanywa kuwa na uzuri usiokuwa na kifani Peponi. Ikiwa mwanamke alikuwa na waume wengi duniani atapewa khiyari kati yao. Atamchagua yule aliyekuwa na tabia nzuri zaidi kuliko wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-6.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020