Swali: Je, aliyeritadi analazimika kulipa swalah na swawm ikiwa atarudi katika Uislamu na akatubia kwa Allaah?
Jibu: Hakuna juu yake kulipa. Mwenye kutubia, Allaah humkubalia tawbah yake. Ikiwa mtu aliacha swalah au akafanya moja ya vichenguzi vya Uislamu kisha Allaah akamuongoza akatubia, basi hahitaji kulipa. Haya ndio maoni sahihi katika maoni ya wanazuoni, kwa sababu Uislamu unafuta yaliyokuwa kabla yake na tawbah hubomoa yaliyokuwa kabla yake. Aidha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ
“Waambie wale waliokufuru kwamba wakikoma watasamehewa yaliyotangulia.”[1]
Kwa hivyo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akabainisha kwamba ikiwa kafiri atakubali Uislamu, basi atamsamehe yale yaliyotangulia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tawbah hufuta yaliyokuwa kabla yake na Uislamu hubomoa yaliyokuwa kabla yake.”
[1]8:38
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/198)
- Imechapishwa: 24/02/2026
Swali: Je, aliyeritadi analazimika kulipa swalah na swawm ikiwa atarudi katika Uislamu na akatubia kwa Allaah?
Jibu: Hakuna juu yake kulipa. Mwenye kutubia, Allaah humkubalia tawbah yake. Ikiwa mtu aliacha swalah au akafanya moja ya vichenguzi vya Uislamu kisha Allaah akamuongoza akatubia, basi hahitaji kulipa. Haya ndio maoni sahihi katika maoni ya wanazuoni, kwa sababu Uislamu unafuta yaliyokuwa kabla yake na tawbah hubomoa yaliyokuwa kabla yake. Aidha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ
“Waambie wale waliokufuru kwamba wakikoma watasamehewa yaliyotangulia.”[1]
Kwa hivyo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) akabainisha kwamba ikiwa kafiri atakubali Uislamu, basi atamsamehe yale yaliyotangulia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tawbah hufuta yaliyokuwa kabla yake na Uislamu hubomoa yaliyokuwa kabla yake.”
[1]8:38
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/198)
Imechapishwa: 24/02/2026
https://firqatunnajia.com/swalah-na-swawm-za-aliyeritadi-baada-ya-kusilimu/