22Ikiwa mwanaume atakutwa akizini na mke wa mtu mwingine, basi wote wawili mwanaume na mwanamke aliyezini naye, ni lazima wauawe. Ni lazima muondoe uovu katika Israel.
23Ikiwa mwanaume atakutana na bikira mjini ambaye ameposwa na mtu akazini naye, 24utawachukua wote wawili kwenye lango la mji na kuwapiga kwa mawe mpaka wafe, yule msichana kwa kuwa alikuwa mjini na hakupiga kelele kuomba msaada, na yule mwanaume kwa sababu amemtenda jeuri mke wa mtu mwingine. Lazima muondoe uovu katikati yenu. 25Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa. 26Usimtendee msichana yule jambo lolote. Hajafanya dhambi inayostahili kifo. Shauri hili ni kama lile la yeyote ambaye anamshambulia na kumuua kwa makusudi jirani yake. 27Kwa maana mwanaume huyo alimkuta msichana huko mashambani, na ingawa msichana aliyeposwa alipiga kelele, hapakuwa na mtu wa kumuokoa.
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kumbukumbu la Torati 22:22-27
- Imechapishwa: 04/11/2017

Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kumbukumbu la Torati 22:22-27
Imechapishwa: 04/11/2017
https://firqatunnajia.com/mzinifu-kupigwa-mawe-katika-biblia/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)