Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… na kila upotevu ni Motoni.”

Kila kitakachozushwa ni Bid´ah na uvumbuzi unaoipoteza dini ya Allaah. Wenye kufanya hivi hawana jengine zaidi ya Moto ikiwa Allaah Hakuwasamehe na wakatubu kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).

Mifumo ya upotevu inaongoza katika Moto na tunaomba kinga kwa Allaah. Kadhalika Bid´ah inawaongoza watu wake katika Moto. Upande mwingine Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) vinaongoza katika Pepo:

وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

“Allaah anaitia nyumba ya amani na Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.” (10:25)

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/219)
  • Imechapishwa: 26/08/2020