31. Dalili ya kwamba Allaah yuko juu, amelingana juu ya ´Arshi

Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Ta´ala) amesema:

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

”Je, mnadhani mko katika amani na Aliyeko mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko katika amani na Aliyeko mbinguni kwamba hatokutumieni kimbunga [cha mawe], basi mtajua vipi [makali] maonyo Yangu.”? (67:16-18)

MAELEZO

Maana ya (فِي السَّمَاء), kwa maana juu. Naye ni Allaah (Jalla wa ´Alaa). Imesemekana vilevile ya kwamba (السَّمَاء), maana yake ni zile mbingu. Kadhalika maana ya (فِي) kwa maana juu. Kwa hivyo maana yake inafika inakuwa juu ya mbingu. Ikisemwa kuwa (السَّمَاء) maana yake ni juu maana yake inakuwa wazi. Hivyo inakuwa ya kwamba (Jalla wa ´Alaa) yuko juu. Vilevile ikisemwa (السَّمَاء) maana yake ni zile mbingu zilizojengwa maana yake inakuwa ´yuko juu ya mbingu`. Kwa sababu (فِي) wakati mwingine inakuja ikiwa na maana ya “juu”. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Fir´awn:

وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ

“Nitakusulubuni (فِي) katika mashina ya mitende.” (20:71)

Bi maana juu ya mashina ya mitende. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema tena:

فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ

“Basi tembeeni (فِي) katika ardhi… ” (09:02)

Bi maana juu ya ardhi. Kwa hivyo kusema kuwa Allaah yuko mbinguni maana yake ni kwamba yuko juu yake na Yeye (Jalla wa ´Alaa) yuko juu ya kila kitu. Haya ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wanasema kuwa yuko juu na kwamba yuko juu ya ´Arshi. Hivo ni tofauti na watu wa Bid´ah miongoni mwa Khawaarij, Mu´tazilah, Jahmiyyah na wengineo. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amejithibitishia Mwenyewe kuwa juu na kwamba yuko juu ya ´Arshi.

Ahl-ul-Bid´ah ndio wenye kusema kuwa Allaah yuko kila mahali. Huu ni ujinga, batili na kufuru. Wanayoamini Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wenye kuwafuata kwa wema ni kwamba Yeye (Subhaanah) ni Mwenye kusifika kuwa juu ya ´Arshi na kwamba amelingana juu yake, kwa msemo mwingine yuko juu yake ujuu ambao unalingana na utukufu Wake. Hafanani na viumbe Vyake katika kitu katika sifa Zake.

Wakati Imaam Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah) – ambaye alikuwa ndiye mwanachuoni mkubwa wa Madiynah katika wakati wake – alipoulizwa juu ya hili akajibu kwa kusema:

“Kulingana kunajulikana. Namna haijulikani. Kuamini hilo ni wajibu. Kuuliza kuhusu hilo ni Bid´ah.”

Vivyo hivyo imepokelewa kutoka kwa mwalimu wake Rabiy´ah bin Abiy ´Abdir-Rahmaan, Umm Salamah, al-Awzaa´iy, ath-Thawriy, Ishaaq bin Raahuuyah, Imaam Ahmad bin Hanbal na maimamu wengine wa Salaf.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 22/10/2024