30. Maafikiano ya Ahl-us-Sunnah kuhusu Allaah kuwa juu ya ´Arshi

Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ

“Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.” (03:55)

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ

”Bali Allaah alimnyanyua Kwake.” (04:158)

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake Yeye linapanda neno zuri na kitendo chema hukinyanyua.” (35:10)

يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَأَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا

“Ee Haamaan! Nijengee mnara mkubwa ili nifikie njia, njia za mbinguni ili nimchungulie mungu wa Muusa. – Kwani hakika mimi namdhania ni mwongo.” (40:36-37)

MAELEZO

Aayah hizi zilizotajwa na mtunzi (Rahimahu Allaah) za mwanzo zinazozungumzia kuhusu ujuu, za nyuma zinazungumzia upamoja.

Allaah (Jalla wa ´Alaa) amejithibitishia Mwenyewe ujuu, kwamba yuko juu ya ´Arshi, yuko juu ya mbingu (Jalla wa ´Alaa) na kwamba anaombwa kutokea kwa juu. Ahl-us-Sunnah wameafikiana juu ya hilo. Ahl-us-Sunnah wameafikiana ya kwamba Allaah (Subhaanah) yuko juu, kwamba yuko juu ya ´Arshi na kwamba amelingana kulingana ambako kunalingana na utukufu na ukubwa Wake. Amesema (Subhaanah):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.” (20:05)

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi.” (07:54)

Kuna Aayah saba ambazo zote (Subhaanah) amethibitisha ujuu na kwamba amelingana juu ya ´Arshi (Jalla wa ´Alaa). Ni kulingana ambako kunalingana na utukufu Wake. Hafanani na viumbe Vyake katika kitu chochote katika sifa Zake. Ni dalili yenye kuonyesha ujuu. Kwa ajili hii ndio maana (Jalla wa ´Alaa) amesema:

يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ

“Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha Kwangu.”

بَل رَّفَعَهُ اللَّـهُ إِلَيْهِ

”Bali Allaah alimnyanyua Kwake.”

Bi maana ´Iysaa (´alayhis-Salaam). Amesema (Jalla wa ´Alaa):

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake Yeye linapanda neno zuri na kitendo chema hukinyanyua.”

Neno “kupanda” na “kunyanyuliwa” ni dalili yenye kufahamisha ujuu. Matendo hupandishwa na neno zuri hunyanyuliwa Kwake. Vilevile Malaika hupanda Kwake. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ

“Malaika na Roho [Jibrily] wanapanda Kwake katika siku kiasi chake ni miaka khamsini elfu.” (70:04)

Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipandishwa Kwake mpaka akavuka mbingu ya saba na akasikia maneno ya Mola (Jalla wa ´Alaa). Yote haya ni haki kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ni wajibu kumthibitishia Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 46-47
  • Imechapishwa: 22/10/2024