29. Dalili juu ya ukamilifu wa Allaah wa uola, ufalme na ujuzi Wake

Shaykh-ul-Isaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ ۖوَكَبِّرْهُ تَكْبِيرًا

”Na sema: “Sifa njema zote ni za Allaah ambaye hakujifanyia mwana na wala hakuwa na mshirika katika ufalme na wala hakuwa dhaifu hata awe [ahitaji] mlinzi; basi mtukuze matukuzo makubwa kabisa.” (17:111)

يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Vinamtakasa Allaah vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini; ufalme ni Wake na sifa njema ni Zake  Naye juu ya kila jambo ni muweza.” (64:01)

تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ نَذِيرًاالَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا

”Amebarikika Yule ambaye ameteremsha Pambanuzi kwa mja Wake ili awe muonyaji kwa walimwengu, Ambaye ni Wake pekee ufalme wa mbingu na ardhi na hakujichukulia mtoto na wala hakuwa na mshirika katika ufalme; na ameumba kila kitu kisha akakikadiria kipimo sawa sawa.” (25:01-02)

مَا اتَّخَذَ اللَّـهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَـٰهٍ ۚ إِذًا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَـٰهٍ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يَصِفُونَ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

”Allaah hakuchukua mtoto yeyote na wala hakukuwa pamoja Naye mungu mwengine. Hapo bila shaka kila mungu angelichukua vile alivyoviumba na baadhi yao wangeliwashinda wengineo. Ametakasika Allaah kutokana na yale yote wanayoyaelezea. Ni Mjuzi wa ghaibu na ya dhahiri. Basi ametukuka kutokana na yale wanayomshirikisha.” (23:91-92)

قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

”Sema: “Hakika si vyenginevyo Mola wangu ameharamisha machafu yaliyodhihirika na yaliyo ya siri na dhambi ukandamizaji bila ya haki na kumshirikisha Allaah kwa chochote kile ambayo hakukiteremshia dalili na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui”.” (07:33)

MAELEZO

Vivyo hivyo amesema (´Azza wa Jall):

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ

”Na sema: “Sifa njema zote ni za Allaah ambaye hakujifanyia mwana na wala hakuwa na mshirika katika ufalme na wala hakuwa dhaifu hata awe [ahitaji] mlinzi!”

Allaah hana mlinzi kutokana na udhaifu. Allaah anao mawalii. Lakini hata hivyo sio walinzi katika ufalme Wake. Yeye ni Mwenye kujitosheleza na kila asiyekuwa Yeye. Yeye ni Mwenye nguvu, Aliye juu na Mshindi. Hana washirika katika ufalme. Pamoja na hivyo ana mawalii Anaowapenda na wao wanampenda. Yule mwenye kumtii na kumcha ndio walii Wake kwa njia ya kwamba Allaah anakuwa ni mwenye kuwapenda na kuwakurubia, kwa sababu wamemtii na kuadhimisha maamrisho Yake. Amesema (Ta´ala):

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ

“Tanabahi! Hakika mawalii wa Allaah hawana khofu juu yao na wala hawatohuzunika, ambao wameamini na wakamcha.” (10:62:63)

Hawa ndio mawalii wa Allaah. Lakini hata hivyo sio wasaidizi katika ufalme. Ni mawalii kwa njia ya mapenzi, kwa sababu wamemtii na kufuata Shari´ah ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Vilevile inahusiana na Aayah nyenginezo zenye kutaja ufalme, sifa kamilifu na uwezo. Hakika Yeye ndiye Mfalme juu ya kila kitu, Muumbaji wa kila kitu, Muweza juu ya kila kitu na ni Mjuzi wa hali zote za waja. Yote haya ni haki. Miongozi mwazo ni pamoja na:

وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا

“… na hakujichukulia mtoto.”

وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

“… na wala hana yeyote anayefanana [wala kulingana] Naye.”akikadiria kipimo sawa sawa

Sifa zote hizi ni zimethibiti Kwake (Jalla wa ´Alaa). Yeye ndiye Muumbaji wa kila kitu:

وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا

“… na ameumba kila kitu kisha akakikadiria kipimo sawa sawa.”

Yeye anazijua hali zote zinazowapitikia waja Wake:

يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Vinamtakasa Allaah vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini; ufalme ni Wake na sifa njema ni Zake  Naye juu ya kila jambo ni muweza.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waaswitwiyyah, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 21/10/2024