Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) sade:

Amesema (Ta´ala):

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ

“Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika na itolewe hukumu?” (02:210)

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّك

”Je, wanangojea jingine lolote isipokuwa wawafikie Malaika au awafikie Mola wako au ziwajie baadhi za alama za Mola wako?” (06:158)

كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

”Sivyo hivyo! [Kumbukeni pale] ardhi itakapovunjwavunjwa, na atakapokuja Mola wako na Malaika safu kwa safu.” (89:21-22)

وَيَوْمَ تَشَقَّقُ السَّمَاءُ بِالْغَمَامِ وَنُزِّلَ الْمَلَائِكَةُ تَنزِيلًا

”Na [kumbusha] Siku itakayopasuka mbingu kwa [kutoa] mawingu na Malaika watateremshwa mteremsho wa wingi.” (25:25)

MAELEZO

Aayah zote hizi tukufu ndani yake mna jumla ya sifa za Mola (´Azza wa Jall). Ni lazima kumthibitishia nazo Allaah (Subhaanah) kwa njia inayolingana Naye pasi na upotoshaji, ukanushaji, kuzifanyia namna wala kuzilinganisha. Miongoni mwazo ni pamoja na maneno Yake (Jalla wa ´Alaa):

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ وَقُضِيَ الْأَمْرُ

“Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika na itolewe hukumu?”

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ أَوْ يَأْتِيَ بَعْضُ آيَاتِ رَبِّك

”Je, wanangojea jingine lolote isipokuwa wawafikie Malaika au awafikie Mola wako au ziwajie baadhi za alama za Mola wako?”

كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا

”Sivyo hivyo! [Kumbukeni pale] ardhi itakapovunjwavunjwa, na atakapokuja Mola wako na Malaika safu kwa safu.”

Ni kuhusu kuja kwa Allaah siku ya Qiyaamah. Ujio siku ya Qiyaamah ni haki kwa njia inayolingana na Allaah. Allaah hashabihiani na viumbe Vyake kwa chochote katika sifa Zake. Amesema (Ta´ala):

أَوْ يَأْتِيَ رَبُّكَ

”… au ziwajie baadhi za alama za Mola wako” (06:158)

Ni kuchomoza kwa jua kutoka magharibi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waaswitwiyyah, uk. 35-37
  • Imechapishwa: 21/10/2024