Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) sade:

Amesema (Ta´ala):

رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

”Allaah Ataridhika nao, nao wataridhika Naye.” (98:08)

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

”Na atakayemuua muumini kwa kusudi, basi malipo yake ni [Moto wa] Jahannam, atakaa humo kwa muda mrefu na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamuandalia adhabu kuu.”(04:93)

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللَّـهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

”Hivyo kwa kuwa wao wamefuata yale yanayomghadhibisha Allaah na wakachukia radhi Zake, basi akayabatilisha matendo yao.” (47:28)

فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ

”Basi walipotukasirisha; Tuliwapatiliza.” (43:55)

وَلَـٰكِن كَرِهَ اللَّـهُ انبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ

”Lakini Allaah amechukia kutoka kwao, basi akawazuia.” (09:46)

كَبُرَ مَقْتًا عِندَ اللَّـهِ أَن تَقُولُوا مَا لَا تَفْعَلُونَ

”Ni chukizo kubwa mno mbele ya Allaah kwamba mnasema yale msiyoyafanya.” (61:03)

MAELEZO

Kughadhibika kunajulikana ambako ni kinyume na kuridhia. Kupenda ni kinyume na kukasirika. Huruma ni kinyume na kupatiliza. Allaah anasifa nazo. Allaah huwahurumia baadhi ya watu na akawaadhibu wengine na wengine akawapatiliza. Huwahurumia watu wenye kupigana katika njia Yake na wengine akawaghadhikia na kuwapatiliza kwa kumuasi na kumkufuru. Hali ni namna hii ambapo Allaah anawapenda baadhi ya watu na wengine anawachukia, anawapa baadhi na wengine anawanyima. Yeye ndiye mwenye kuzuia na kutoa (Jalla wa ´Alaa).

Huu ndio mfumo wa Ahl-us-Sunnah. Wanaziamini sifa na wakati huohuo wanaamini kuwa ni haki, kwamba zinalingana na Allaah na kwamba maana yake ni haki. Lakini hakuna anayejua namna yake isipokuwa Yeye Mwenyewe (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waaswitwiyyah, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 21/10/2024