575- Nilimsikia Ahmad akiulizwa kuhusu bwana mmoja ambaye anatoa zakaah kumpa mwanae. Akajibu: “Asimpe mwanae, mtoto wa mvulana wake wala mtoto wa msichana wake, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kuhusu al-Hasan (Radhiya Allaahu ´anh):

“Hakika mtoto wangu huyu ni bwana na Allaah atayakusanya makundi mawili ya waislamu yanayopigana kupitia kwake.”[1]

Amemwita mtoto. Wala haifai akatoa zakaah kuwapa wazazi wake.

[1] al-Bukhaariy (3/243).

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 119
  • Imechapishwa: 20/02/2021