Wanandoa kutia saini serikalini ya kuchangia umiliki

Swali: Swali hili ni kutoka Tunisia. Nimejiwa na kijana na nimemkubali. Tumefunga ndoa ya Kishari´ah na bado hatujafanya ndoa ya serikali. Na sisi Tunisia wakati wa kufanya hatua ya ndoa ya serikali tuna khiyari mbili ili itimie ndoa hii. 1) Aidha mwanamke na mwanaume watie saini, nayo ni kushirikiana katika umiliki. Yaani kila kitakachopatikana baada ya ndoa tunakichangia sisi sote. 2) Khiyari ya pili ni kwamba kila mmoja ana mali zake binafsi na wala hawachangii lolote. Ni ipi katika hizi mbili inayoafikiana na Shari´ah ili tuitilie saini?

Jibu: Ninawanasihi kwa hii ya pili. Ama ya kwanza ni katika natija za kanuni zilizotungwa. Laana ya Allaah iwe juu yazo na juu ya walioziunda na kuzihalalisha.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/4187
  • Imechapishwa: 22/09/2020