Wanafunzi zaidi ya 900 wanaruhusiwa kuswali chuoni?

Swali: Wanafunzi wa masomo ikiwa idadi yao wanazidi wanafunzi 900 inafaa kwao wakaswali masomoni ikiwa msikiti umekurubiana na ukuta wa masomo?

Jibu: Wanatakiwa kuswali msikitini ikiwa nafasi ya msikiti inawatosha. Waalimu wao wanapaswa kuwatilia mkazo ili watekeleze swalah msikitini.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 12/02/2021