Swali: Kuna mwanaume anayeswali amemposa mwanamke ambaye anaswali. Baba yake ambaye amemuoza haswali. Je, ndoa ni sahihi?

Jibu: Baba ambaye haswali hana usimamizi kwa mwanamke ambaye anaswali. Kwa kuwa huyo mwanamke ni Muislamu na baba yake ni kafiri. Kutokana na kauli sahihi [katika kauli za wanachuoni]. Kwa hivyo inatakikana na ni jambo la wajibu avuliwe usimamizi kutoka kwake [huyo baba yake] na uchukue wengine. Kwa mfano yuko na kaka anayeswali, ami anayeswali. Usimamizi unawaendea watu hawa. La sivyo ajulishwe kauli ya kutosihi kwa ndoa, kwa kuwa hali yako haistahiki kuwa msimamizi kwa mwanamke huyu isipokuwa mpaka ujadidi Uislamu wako na uswali. Akifanya hivyo hapo ndipo ndoa itakuwa ni sahihi, na kama hakufanya hivyo, hapana.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alnajmi.net/voices.php?action=show&id=167
  • Imechapishwa: 22/09/2020