Kitabu cha Allaah kiko mbele yetu na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ziko mbele yetu. Ubainifu wake kutoka kwa Mtume wa Allaah ni kitu kiko wazi na ´Aqiydah ya Salaf iko wazi. Allaah amejaalia vimechapishwa na kuenezwa. Miongoni mwa vitabu hivyo ni pamoja na hivi vifuatavyo:

1- “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy.

2- “as-Swahiyh” ya Muslim.

3- Tafsiyr ya Qur-aan ya Ibn Jariyr [at-Twabariy].

4- Tafsiyr ya Qur-aan ya Ibn Kathiyr.

5- “as-Sunnah” ya ´Abdullaah bin Ahmad.

6- “as-Sunnah” ya Ahmad [bin Hanbal].

7- “Kitaab-ut-Tawhiyd” ya Ibn Khuzaymah.

8- “Sharh Usuwl-il-I´tiqaad Ahl-us-Sunnah” ya al-Lalakaa´iy.

9- “Ibaanat-ul-Kubrah was-Sughrah” ya Ibn Battwah.

10- “ash-Shariy´ah” ya al-Aajurriy.

Vitabu hivi ndivyo vinavoyiwakilisha njia ya waumini kwa uwakilisho wa wazi kabisa usiokuwa na utata. Hivyo basi, ni juu yetu kusoma vitabu hivi ili tujue njia ya waumini na itubainikie njia ya waovu. Kupitia vitabu hivi itatubaikia njia ya waumini na kufichuka njia ya waovu. Ni wingi ulioje wa njia ambazo zinaweza kuteuliwa kuwekwa katika njia ya waovu!

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=7539
  • Imechapishwa: 06/09/2020