Vipi mtu ataswali ndani ya ndege?

Swali: Mtu akiingia ndani ya ndege kabla ya kuingia wakati, kisha akiwa ndani ya ndege ukaingia wakati wa swalah – anatakiwa kuiswali kwa sifa na namna gani?

Jibu: Kama ilivyotangulia: ikiwezekana kusubiri mpaka atue na kuswali ndani ya wakati, basi asubiri ili aswali swalah ya faradhi kwa sifa yake iliyowekwa katika Shari´ah. Lakini kama hilo halijawezekana, basi ataswali kulingana na hali yake:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Ataswali kuelekea upande wa Qiblah na ataenda pamoja na mwelekeo wa ndege katika swalah ya faradhi. Ama sunnah, basi ataswali kulingana na hali yake. Ataswali kwa mwelekeo wa safari ya ndege katika swalah zinazopendeza. Ama faradhi lazima aelekee Qiblah, ataswali kuelekea Qiblah na ataenda pamoja na mwelekeo wa ndege. Atarukuu na kusujudu akiwa angani, huku Sujuud ikawa chini zaidi kuliko Rukuu´.

[1] 64:16

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31710/ما-كيفية-صلاة-المسافر-في-الطاىرة
  • Imechapishwa: 02/12/2025