Unachotakiwa kufanya ukitilia mashaka ya kufanya nguzo moja wapo ya swalah

Swali: Mwenye kuswali peke yake akitilia mashaka kama amesoma al-Faatihah au hakusoma – je, alipe Rak´ah nyingine au asujudu [sijda ya kusahau]?

Jibu: Hapana. Akitilia mashaka juu ya kusoma al-Faatihah ni kama kwamba hakuisoma. Akitilia mashaka ya kuacha nguzo basi ameiacha. Akitilia mashaka juu ya Rukuu´ au Sujuud ni kama kwamba hakuifanya. Kwa hivyo anapaswa kuileta. Isipokuwa akiwa ni mtu mwenye wasiwasi sana. Katika hali hiyo atapuuza mashaka hayo. Ama akiwa ni mtu wa kawaida na si mwenye wasiwasi sana akiwa na mashaka ya kuacha nguzo ni kama ameiacha. Hivyo atatakiwa kuileta. Ni lazima kuileta.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/89/%D8%B4%D9%83-%D9%81%D9%8A-%D9%82%D8%B1%D8%A7%D8%A1%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%81%D8%A7%D8%AA%D8%AD%D8%A9
  • Imechapishwa: 08/12/2019