Swali: Mtu mmoja amesafiri kwenda nje kwa ajili ya jukumu la masomo na alilazimishwa kufanya hivyo. Hajaoa bado na ana khofu juu ya nafsi yake. Je, inajuzu kwake kuoa huko, huku akiwa na nia moyoni mwake kuwa atamwacha mke huyo atakaporejea katika nchi yake, bila ya kuwajulisha watu wa upande wa mke?
Jibu: Hakuna tatizo katika jambo hili ikiwa ataoa katika sehemu ya safari na moyoni mwake ana nia kuwa atamwacha akitaka kurejea, hakuna tatizo kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi. Baadhi ya wanazuoni wamechukua msimamo wa kusimama katika suala hili wakiogopa kuwa huenda ikawa ni katika aina ya ndoa ya starehe. Hata hivyo mambo sivyo. Mingoni mwa sharti za ndoa ya starehe ni kwamba inafungwa hadi muda maalum; kwa namna ya kwamba mtu anaoa kwa sharti kwamba atamwacha baada ya mwezi, miwili au mitatu na kwamba baada ya muda huo hakuna tena ndoa baina yao. Hiyo ndiyo ndoa ya starehe. Ama ndoa ya kawaida isiyo na sharti la muda, isipokuwa tu mtu ana ameweka nia moyoni mwake kuwa atamwacha mke huyo atakaposafiri kutoka katika nchi hiyo, hii si ndoa ya starehe. Huenda akamwacha au akapendezewa naye akaendelea naye. Kwa hivyo si katika mlango wa ndoa ya starehe kwa mujibu wa maoni sahihi. Huo ndio msimamo wa wanazuoni wengi – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30006/حكم-الزواج-بنية-انه-سيطلقها-عندما-يسافر
- Imechapishwa: 27/08/2025
Swali: Mtu mmoja amesafiri kwenda nje kwa ajili ya jukumu la masomo na alilazimishwa kufanya hivyo. Hajaoa bado na ana khofu juu ya nafsi yake. Je, inajuzu kwake kuoa huko, huku akiwa na nia moyoni mwake kuwa atamwacha mke huyo atakaporejea katika nchi yake, bila ya kuwajulisha watu wa upande wa mke?
Jibu: Hakuna tatizo katika jambo hili ikiwa ataoa katika sehemu ya safari na moyoni mwake ana nia kuwa atamwacha akitaka kurejea, hakuna tatizo kwa mujibu wa maoni ya wanazuoni wengi. Baadhi ya wanazuoni wamechukua msimamo wa kusimama katika suala hili wakiogopa kuwa huenda ikawa ni katika aina ya ndoa ya starehe. Hata hivyo mambo sivyo. Mingoni mwa sharti za ndoa ya starehe ni kwamba inafungwa hadi muda maalum; kwa namna ya kwamba mtu anaoa kwa sharti kwamba atamwacha baada ya mwezi, miwili au mitatu na kwamba baada ya muda huo hakuna tena ndoa baina yao. Hiyo ndiyo ndoa ya starehe. Ama ndoa ya kawaida isiyo na sharti la muda, isipokuwa tu mtu ana ameweka nia moyoni mwake kuwa atamwacha mke huyo atakaposafiri kutoka katika nchi hiyo, hii si ndoa ya starehe. Huenda akamwacha au akapendezewa naye akaendelea naye. Kwa hivyo si katika mlango wa ndoa ya starehe kwa mujibu wa maoni sahihi. Huo ndio msimamo wa wanazuoni wengi – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30006/حكم-الزواج-بنية-انه-سيطلقها-عندما-يسافر
Imechapishwa: 27/08/2025
https://firqatunnajia.com/tofauti-ya-ndoa-ya-starehe-na-ndoa-ambayo-mtu-ameweka-nia-ya-kumwacha-mke-haja-itakapomalizika/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket