Swalah alizoacha kwa kipindi cha siku 1,5 wakati hedhi ilipokatika

Swali: Kuna mwanamke alipata ada ya mwezi katika wakati wake. Lakini mwanzoni mwa ada hiyo alimjia damu kidogo kisha ikasita kwa muda wa siku moja na nusu, kisha damu ikamrejelea kwa mara nyingine na ikaendelea mpaka zikamalizika zile siku zake za ada na akasafika. Je, zile swalah alizoacha katika kile kipindi cha siku moja na nusu ni lazima azilipe?

Jibu: Kama alikuwa hana damu kabisa analazimika kuzilipa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-07-03-1438-هـ
  • Imechapishwa: 20/06/2022