Swali: Wanajuzisha baadhi ya watu maandamano ya amani dhidi ya mtawala ambaye kakufuru na wanatumia hoja kwa kusema wanachuoni wamejuzisha hilo. Je, maoni yao hii ni sahihi?

Jibu: Wanachuoni wamejuzisha tu kufanya uasi kwa mtawala ambaye ni kafiri dalili ziko wazi kama lionekanavyo juwa. Mpaka muone ukafiri wa wazi kabisa wenye dalili kwa Allaah. Demokrasia inaharibu Uislamu na si katika Uislamu. Maandamano si katika Uislamu. Na Waislamu hawafai kufanya matendo kama haya. Kinachohitajika ni subira wakati wa fitina na dhuluma za mtawala. Mpaka hapo Allaah (Ta´ala) atapoleta nusura. Na kuna kitabu – makala nimeandika kuhusiana na hili, wape ndugu wakisome na wajue hukumu za Kishari´ah kwa demokrasia hizi na haya maandamano. Mtajua hilo kwa dalili. Na nimebainisha upotofu wa wanaosema kuwa ni katika Uislamu na ni katika kuamrisha mema na kukataza maovu. Madai haya ni batili na si katika Uislamu. Bali katika Uislamu ni subira, kama alivyotueleza hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na nimetaja kwa dalili katika makala hii na mstaftafidi kwa jibu hili.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=SI3eQTaASkg
  • Imechapishwa: 06/09/2020