Pato la haramu kwa shangazi mgonjwa na muhitaji

Swali: Nilipata mali kwa njia ya haramu. Je, inajuzu kumpa nazo shangazi yangu ambaye ni fakiri na ni mgonjwa ili niweze kujinasua nazo?

Jibu: Ikiwa umetubu kwa Allaah kwa kitendo hichi mpe nazo muhitaji, ni mamoja ikiwa ni ndugu yako au mwingine. Unafanya hivo ili uweze kujikwamua nazo, na si kwa ajili ya kutoa swadaqah. Hii ni kama mali iliyopotea asiyopatikana mmiliki wake; mpe yule anayehitajia. Hata hivyo unatakiwa kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Ama kusema uendelee kuchuma pato la haramu na kulitoa swadaqah ni haramu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–09041434.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020