Nimwambie mposaji marafiki wa kiume niliokuwa nao?

Swali: Dada kutoka Tunisia anauliza. Alikuwa na uhusiano wa kiharamu kinyume na Shari´ah na mtoto wa ami yake. Anajua kuwa alikuwa mkosevu. Na kwa sasa amechumbiwa na mwanaume mwingine. Je, ni wajibu kwake kumueleza yaliyopitika au hapana?

Jibu: Jambo la kwanza ewe dada kutoka Tunisia, ninamuomba Allaah akuneemeshe tawbah ya kweli na pengine ulitubia na hili ndilo linalodhihiri katika swali lako. Hakika tawbah ya kweli inafuta yaliyotangulia.

Jambo la pili, mimi sijui, je ulikuwa na mume au bikira? Ikiwa ulikuwa na mume kisha akakutaliki, isitiri nafsi yako. Ikiwa ulikuwa na mume, ukapitikiwa na yanayompitikia mwanamke kutoka kwa mume wake, kisha mume huyu akakutaliki au akafa, isitiri nafsi yako na wala usimwambie lolote. Ama ikiwa uko bikira kama alivyoiumba Allaah, nakuusia umwambie kwamba ilinipitikia mchezo na ikaondoka bikira. Nielewe makusudio yangu, ikaondoka. Muwekee wazi ili awe anajua hilo. Na wala usimwambie yanayochukiza.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/6390
  • Imechapishwa: 22/09/2020