Nimtii mume anayetaka nisafiri bila Mahram?

Swali: Mimi naishi Saudi Arabia na mke wangu anaishi mji mwingine. Mume anataka mke wake asafiri peke yake kwa kutumia hoja kwamba ni mke wake na ni lazima kwake kumtii na kuko mtu ambaye ametoa fatwa hiyo kujuzu kusafiri bila ya kuwa na Mahram. Je, inajuzu kwangu kumtii?

Jibu: Hapana.

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Sawa ikiwa ni mume, baba wala kiumbe yeyote:

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

Mwanamke kusafiri bila ya Mahram ni maasi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Si halali… “

Ni nini maana ya si halali? Maana yake ni kwamba ni haramu na ni maasi.

“Si halali kwa mwanamke kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Asimtii mume wake katika hili. Hata kama atafutu mwenye kufutu amekwenda kinyume na dalili. Aliyetoa Fatwa hii amekosea na ameenda kinyume na dalili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14340428.mp3
  • Imechapishwa: 20/09/2020