Swali 295: Mwanaume akimuoa mwanamke bikira kisha asione ubikira wake – amsitiri au afanye nini?

Jibu: Swali hili ni zuri na muhimu sana. Kwa nini, enyi ndugu zangu? Kwa sababu watu huenda kweli wanafuata mwenendo huu wa kijinga. Inapaswa itambulike ya kwamba wanachuoni, bali hata madaktari pia, wametaja sababu za kuondoka ubikira. Wakati mmoja ubikira unaweza kuwa imara na wakati mwingine vilevile unaweza kuondoka. Kwa mfano huenda akakimbia na akaanguka kichalichali na hivyo ukaondoka ubikira wake, huenda kwa sababu ya kupata kwa wingi ada ya mwezi, huenda aliteleza wakati wa kufanya michezo pamoja na watoto wake utotoni kabla ya kubaleghe na sababu nyenginezo. Kwa hivyo mtu anapomuoa mwanamke ambaye ni bikira na asimuone kuwa ni bikira, basi anapaswa kufanya yafuatayo: akiwa ni mwenye kuelewa na anaweza kuidhibiti basi yake na akamtafutia nyudhuru, ana haki ya kufanya hivo. Vinginevyo ni lazima kwake kumsitiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumsitiri muislamu basi Allaah atamsitiri.”

Ni haramu tena ni haramu juu yake kueneza kati ya watu kwamba ameuondosha bikira yake. Kwa sababu kuondoka kwa ubikira kunaweza kutokamana na sababu nyenginezo mbali na uzinzi kama ambavyo kuna uwezekano vilevile akawa alibakwa na sababu  nyenginezo ambazo mnazijua.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 538
  • Imechapishwa: 06/12/2019