Ni ipi hukumu ya kumswalia maiti makaburini kwa wale waliopitwa na swalah?

Swali: Ni ipi hukumu ya kumswalia maiti makaburini kwa yule ambaye hakumswalia?

Jibu: Sijui Sunnah yoyote juu ya hilo kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah. Lakini linaingia katika jumla ya makokotezo ya kumswalia maiti. Mtu anaweza kutumia hilo dalili vilevile kwa kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi aliposwalia kaburi la mwanamke aliyekuwa akifuagia msikiti.

Mtu akija ilihali ameshapitwa na swalah msikitini amswalie na haina neno. Anapata ujira – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/140)
  • Imechapishwa: 15/09/2021