Nasaha za al-Waadi´iy kwa Salafiyyuun juu ya propaganda za Hizbiyyuun

Baada ya kusoma kitabu ”al-Khutwutw al-´Ariydhwah fiy Ad´iyaa’-is-Salafiyyah” cha ash-Shaayijiy nimetambua kuwa ni mtu fasiki na asiyejali jambo la Uislamu, waislamu wala kuwasemea uongo walinganizi wanaolingania kwa Allaah. Haya niliyaona kabla ya kusoma Radd ya ndugu yetu Faalih bin Jabr juu yake. Allaah amjaze kheri. Amemnukuu kutoka kwenye magazeti na majarida. Ikaonekana kuwa mtu ni fasiki na haitakikani kumjali wala vitabu vyake. Huyu pengine ametumwa na shaytwaan. Si mwenye kuongeze chumvi katika jambo hili. Dalili ya hilo ni kwamba Hizbiyyun hapa walikuwa wakijikombakomba kwa naibu wa raisi ´Aliy Saalim al-Baydhw. al-Ikhwaan al-Muslimuun na wengineo walikuwa wakijikombakomba kwake. Sambamba na hilo Ahl-us-Sunnah walikuwa imara; mkomunisti ni mkomunisti na ni kafiri tangu hapo kale na daima.

Endeleeni kulingania. Vitabu na vipeperushi hivi vitakuwa vyenye kuinusuru Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni lazima kwa ndugu zenu kuwatembelea ndugu zao na kuwapa anasa, ijapo watabaki kwa kiasi cha mwezi, ili waweze kuwasaidia ndugu zao kutoka katika Ahl-us-Sunnah. Msivunjike moyo. Msiwajali yale yanayosemwa. Nyinyi ndio mko katika haki. Haki itakuja kushinda leo au kesho. Mola anasema katika Kitabu Chake kitukufu:

بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ

“Bali Tunaitupa haki juu ya batili inaitengua, tahamaki [batili hiyo inakuwa] ni yenye kutoweka.” (21:18)

وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ ۚ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا

“Na sema: “Haki imekuja na ubatilifu umetoweka. Hakika ubatilifu daima ni wenye kutoweka.”” (17:81)

Nyinyi ndio mko katika haki. Uongo na batili zote hizi zitamalizika leo au kesho au kesho kutwa. Sisi tunawazungumzisha Hizbiyyuun kwamba hatuyajali maandiko yao, kazi zao, Khutbah zao wala mikusanyiko yao. Sisi hatuyajali. Hamtuzidishii kitu isipokuwa kushikamana barabara na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wao hawapigi kelele isipokuwa ni kwa sababu wanaona namna ambavo watu wameanza kuwaamini na kuhisi utulivu juu ya ulinganizi wenu. Nyinyi mko katika haki. Allaah akujazeni kheri.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=21
  • Imechapishwa: 10/02/2021