Swali: Vipi inakuwa ndoa ya Kishari´ah?

Jibu: Inakuwa kwa kutimiza masharti yake na nguzo zake. Ndoa ya Kishari´ah ina sharti zake na ina nguzo zake. Zikitimia sharti na nguzo zake hapo ndo inakuwa ya Kishari´ah. Ninamnasihi yule ambaye anataka kuoa ajifunze kwanza Ahkaam za ndoa ili asije kutumbukia katika jambo ambalo linaenda kinyume na Shari´ah ilihali naye hajui. Anasema Allaah:

فَاسْأَلُواْ أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ

“Basi waulizeni wenye kujua kama nyinyi hamjui.” (16:43)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=558
  • Imechapishwa: 22/09/2020