Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuita mfumo wa Salaf kuwa ni mfumo haribifu?

Jibu: Hukumu ni kuwa yeye ndiye muharibifu.

Ndugu! Usishangazwe watu wa kheri kuitwa kwa majina mabaya bandia. Je, hujui kuwa Mitume walisifiwa kuwa ni wachawi na wendawazimu? Allaah (Ta´ala) amesema:

كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ

“Namna hiyo hawakuwafikia kabla yao Mitume isipokuwa walisema: “Mchawi au mwendawazimu.” (51:52)

Je, majina haya yaliwadhuru Mitume? Hapana, mwisho mzuri waliupata wao na Alhamdulillaah. Usishangazwe watu wa kheri wakiitwa majina mabaya. Je, hujui ya kuwa wale wanaopinga sifa za Allaah (´Azza wa Jall) wanawaita wale wenye kuzithibitisha kuwa ni Mujassimah, Hashawiyyah na Nawaabit. Hili haliwadhuru.

Ikiwa ni hivyo ya kwamba Salafiy anakwenda kinyume na manhaj ya Salaf, tunasema kuwa huyu ni muharibifu. Lakini hatunasibishi kosa hili kwa manhaj hii. Tuna ndugu zetu ambao wako katika manhaj ya Salaf, au ambao wanataka manhaj ya Salaf wanaokwenda kinyume na manhaj ya Salaf katika mienendo yao. Wanadhuru Uislamu na waislamu zaidi ya wanavyounufaisha. Inawezekana mtu huyu ameona Salafiy na tabia mbaya. Kwa ajili hiyo akasema kuwa Salaf ndio waharibifu.

Hatujui yaliyopitika. Lakini ikiwa anakusudia Salaf ya kihakika, tunasema:

“Wewe ndiye muharibifu na sio mfumo wa Salaf.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (235)
  • Imechapishwa: 06/09/2020