Swali: Je, mwanamke anaweza kujibia swali alilosikia au kulisoma?

Jibu: Ndio, ikiwa yuko na elimu. Wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakeze wengi wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhunn) walikuwa wakitoa fatwa. Hayo hayo yalifanywa na wanawake wajuzi baada ya Maswahabah. Ikiwa yuko na elimu juu ya Qur-aan na Sunnah ajibu maswali na awafunze watu. Vilevile anaweza kuwanukulia fatwa aliyopata au aliyosikia kwenye redio. Ikiwa amehifadhi kitu awanukulie nacho. Anaweza kufanya hali kadhalika ikiwa amesoma kitu kwenye vitabu vya Ahl-us-Sunnah vinavyojulikana. Lakini inahitajia awe mwanafunzi na awe anaelewa. Awanukulie wengine maana. Yote haya ni katika kushirikiana katika wema na uchaji Allaah, kuinukuu elimu na kulingania katika haki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.binbaz.org.sa/node/10566
  • Imechapishwa: 24/09/2020