Swali: Inajuzu kwa mwanamke ambaye kalazimishwa [kuolewa na] mume na familia yake na wala hampendi mume huyu kuomba Talaka?

Jibu: Jambo la kwanza ni kwamba,kuridhia kwa mke kwa mume [atakae kumuoa] ni jambo la lazima. Bali ni sharti ya kusihi kwa ndoa. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Asiozeshwe bikira mpaka aombwe idhini.”

Ikithibiti kweli ya kwamba kalazimishwa na hakuridhia, arejelewe Qadhiy wa Kishari´ah akate hukumu hiyo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=gTKrzU_2IKY
  • Imechapishwa: 22/09/2020