Swali: Kuna mwanamke mume wake anakataa asiende sokoni na yeye hamletei haja zake na anasema ukienda basi usirudi kwangu. Je, nikienda talaka imepita na lipi la kufanya katika hali kama hii?

Jibu: Talaka inapita ikiwa mume ameinuia. Ikiwa hakuinuia na badala yake amenuia kumtisha [haipiti]. Mara nyingi watu wanaposema hivi wanakusudia kutisha na kwamba mke wake anamuona kuwa ni ghali kwake, na lau atamuasi haonelei kumtaliki. Lakini miongoni mwa watu kuko ambao wanaona lau atamuasi anaona hakuna faida ya kubaki naye na anamtaliki. Hivyo basi tunasema, hakika ya kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia. Mwenye kunuia kumtisha na hakunuia talaka, akimuasi hatalikiki lakini pamoja na hivyo juu yake ana kafara ya yamini. Anapaswa kulisha masikini kumi, kwa kila masikini mmoja karibu kilo moja na nusu. Ama ikiwa amekusudia talaka imepita kwa kuwa kila ´amali inalipwa kutegemea na nia.

Kuhusiana na afanye nini na yeye anahitajia kutoka kwenda sokoni kununua nguo na mume wake anamkatalia, abaki nyumbani mpaka hapo Allaah atapomwongoza na kumruhusu hilo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 02
  • Imechapishwa: 23/09/2020