Swali: Kuna muda kiasi gani kati ya adhaana ya kwanza na adhaana ya pili ya Fajr?
Jibu: Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“… ili arudi aliyesimama kuswali na aamke aliyelala.”
Hivyo haipaswi kuwa muda mrefu. Bali kwa muda mfupi kabla ya alfajiri ili watu waamke; yule anayehitaji kutawadha au aliye katika janaba apate kuoga. Haifai kuadhiniwa mapema sana baada ya katikati ya usiku. Bali iwe karibu na alfajiri ili manufaa ya adhaana yapatikane. Kwa kuwa ikiwa ataadhini mapema mno, basi watu hawatajali. Watapoteza manufaa yake na wataendelea kulala. Lakini ikiwa adhaana ya kwanza itakuwa karibu na alfajiri, basi itamuamsha aliyelala na kumfanya aliyesimama kuswali usiku ajue kuwa alfajiri imekaribia na hivyo atapumzika. Kwa hiyo Sunnah ni kwamba adhaana ya kwanza isicheleweshwe sana kutoka ile ya pili. Kwa sababu hiyo imekuja katika baadhi ya mapokezi ya Hadiyth ya Bilaal (Radhiya Allaahu ´anh):
“Haikuwa kati yao isipokuwa kwamba huyu alipanda na huyu akashuka.”
Kwa maana ya kwamba ilikuwa karibu sana.
Mwanafunzi: Baadhi ya waadhini wanaweka muda wa saa moja kati ya adhaana ya kwanza na ya pili?
Ibn Baaz: Hilo ni kutokana na Ijtihaad yao binafsi. Hakuna dalili ya wazi juu yake. Iwapo ni saa moja au nusu saa, yote ni muda unaokaribiana. Mtu anaweza kuswali Witr katika huo muda.
Mwanafunzi: Imepokelewa katika baadhi ya mapokezi kwamba ni kwa muda wa kusoma Aayah khamsini?
Ibn Baaz: Hapana, hilo ni baina ya adhaana ya Fajr na Iqaamah, si baina ya adhaana mbili.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu adhaana ya ijumaa?
Jibu: Hilo lilifanywa na Maswahabah katika zama za ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na waliokuja baada yake. Aliamuru adhaana ya kwanza itolewe ili kuwazindua watu kwamba ni siku ya ijumaa. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wakaafikiana naye. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jilazimiane na Sunnah zangu na Sunnah ya makhaliyfah waongofu baada yangu.”
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31555/ما-مقدار-الفصل-بين-الاذانين-في-الفجر-والجمعة
- Imechapishwa: 05/11/2025
Swali: Kuna muda kiasi gani kati ya adhaana ya kwanza na adhaana ya pili ya Fajr?
Jibu: Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“… ili arudi aliyesimama kuswali na aamke aliyelala.”
Hivyo haipaswi kuwa muda mrefu. Bali kwa muda mfupi kabla ya alfajiri ili watu waamke; yule anayehitaji kutawadha au aliye katika janaba apate kuoga. Haifai kuadhiniwa mapema sana baada ya katikati ya usiku. Bali iwe karibu na alfajiri ili manufaa ya adhaana yapatikane. Kwa kuwa ikiwa ataadhini mapema mno, basi watu hawatajali. Watapoteza manufaa yake na wataendelea kulala. Lakini ikiwa adhaana ya kwanza itakuwa karibu na alfajiri, basi itamuamsha aliyelala na kumfanya aliyesimama kuswali usiku ajue kuwa alfajiri imekaribia na hivyo atapumzika. Kwa hiyo Sunnah ni kwamba adhaana ya kwanza isicheleweshwe sana kutoka ile ya pili. Kwa sababu hiyo imekuja katika baadhi ya mapokezi ya Hadiyth ya Bilaal (Radhiya Allaahu ´anh):
“Haikuwa kati yao isipokuwa kwamba huyu alipanda na huyu akashuka.”
Kwa maana ya kwamba ilikuwa karibu sana.
Mwanafunzi: Baadhi ya waadhini wanaweka muda wa saa moja kati ya adhaana ya kwanza na ya pili?
Ibn Baaz: Hilo ni kutokana na Ijtihaad yao binafsi. Hakuna dalili ya wazi juu yake. Iwapo ni saa moja au nusu saa, yote ni muda unaokaribiana. Mtu anaweza kuswali Witr katika huo muda.
Mwanafunzi: Imepokelewa katika baadhi ya mapokezi kwamba ni kwa muda wa kusoma Aayah khamsini?
Ibn Baaz: Hapana, hilo ni baina ya adhaana ya Fajr na Iqaamah, si baina ya adhaana mbili.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu adhaana ya ijumaa?
Jibu: Hilo lilifanywa na Maswahabah katika zama za ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) na waliokuja baada yake. Aliamuru adhaana ya kwanza itolewe ili kuwazindua watu kwamba ni siku ya ijumaa. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wakaafikiana naye. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Jilazimiane na Sunnah zangu na Sunnah ya makhaliyfah waongofu baada yangu.”
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31555/ما-مقدار-الفصل-بين-الاذانين-في-الفجر-والجمعة
Imechapishwa: 05/11/2025
https://firqatunnajia.com/muda-baina-ya-adhaana-ya-kwanza-na-adhaana-ya-pili-ya-fajr/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket