Swali: Kuna mtu ni Salafiy lakini ndugu zake kama baba yake, ndugu yake na mjomba wake ni Ikhwaaniyyuun. Vipi atatangamana nao na khaswa inapokuja katika kula pamoja nao?

Jibu: Ninaonelea kuwa aungu udugu nao, lakini ajitahidi kuwalingania. Ikiwa yuko na elimu na wakamletea utata aupige Radd kwa dalili. Upande mwingine ikiwa hana elimu awasiliane na ambaye anaweza kumfichulia utata huu kisha awajibu. Kwa sababu watu hawa wamepewa mtihani na ndugu kama hawa na hawawezi kutengana nao. Katika miji mingi mtu hawezi kutengana na ndugu zake na kuishi mbali na wao. Tofauti na baadhi ya sehemu mtu anaweza kuishi mbali na wao na akawa anawatembelea mara kwa mara.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/11319
  • Imechapishwa: 21/09/2020