Swali: Nifanye nini na mke ambaye amekataa kuvaa mavazi yanayokubalika katika Shari´ah? Je, mume amtaliki au abaki pamoja naye?

Jibu: Ni wajibu kwake kumlazimisha kuvaa mavazi yanayokubalika katika Shari´ah. Akiendelea kuasi, basi amzuie kutoka nje ya nyumba. Kwa sababu yeye ndiye mwenye usimamizi juu yake. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya [matumizi] wanayotoa katika mali zao.”[1]

[1] 04:34

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=wXBXfYCFlh8&app=desktop
  • Imechapishwa: 12/09/2020