Mchelewesahji swalah hapati thawabu wala dhambi

Swali: Nimemsikia mwalimu mmoja wa kike akisema kuwa anayechelewesha swalah ya Dhuhr mpaka kabla ya ´Aswr basi hapati thawabu wala dhambi. Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Kuchelewesha swalah mpaka kabla ya kuingia wakati wa swalah ya pili ni jambo linaloenda kinyume na lililo bora. Amepitwa na ujira wa kuswali swalah ndani ya wakati wake [wa mwanzo]. Lakini haifai kwetu kusema kuwa hapati thawabu wala dhambi. Kwa sababu hilo linaenda kinyume na maandiko mengi sahihi kwa mfano:

“Swalah tano, swalah ya ijumaa mpaka swalah ya ijumaa nyingine inafuta yale yote yaliyoko kati yake… “[1]

”Yule anayemsabihi Allaah mara 33, akamhimidi Allaah mara 33 na akamkabiri Allaah mara 33 baada ya kila swalah, basi Allaah atamsamehe madhambi yake ijapo yatakuwa kama mfano wa mapovu ya bahari.”[2]

Na maandiko mengine.

[1] Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah tano, swalah ya ijumaa mpaka swalah ya ijumaa nyingine na Ramadhaan mpaka Ramadhaan nyingine, inafuta yale yote yaliyoko kati yake midhali mtu anayaepuka yale madhambi makubwa.” (Muslim (02/05)).

[2] Muslim (05/26).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 127
  • Imechapishwa: 01/07/2022