Mambo ambayo kila muislamu anaweza kulingania

Swali: Je, kulingania ni jukumu la kila muislamu au kulingania ni jukumu la watu maalum?

Jibu: Kila muislamu ana jukumu la kulingania kwa kiasi cha uwezo wake. Amesema (Ta´ala):

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.” (16:125)

Kila mmoja vile awezavyo. Unamtahadharisha huyu na maasi, mwingine anamwamrisha jambo la kheri na mwingine anamkataza shari. Kila mmoja anatakiwa kulingania kwa Allaah. Baba anatakiwa kulingania kwa Allaah, baba anatakiwa kulingania kwa Allaah, imamu wa msikiti anatakiwa kulingania kwa Allaah, Khatwiyb anatakiwa kulingania kwa Allaah na mwalimu anatakiwa kulingania kwa Allaah. Kila mtu ambaye nia na kusudio lake ni njema [… sauti haisikiki vizuri…] yuko katika njia ya kheri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/فتاوى-على-الهواء-13-11-1435هـ-0
  • Imechapishwa: 19/06/2022