16 – ´Abdul-Malik bin Qaruub al-Asma´iy amesema:

”´Amr bin ´Ubayd alikuja kwa Abu ´Amr bin al-´Alaa’ na kumuuliza: “Ee Abu ´Amr! Je, Allaah anavunja ahadi yake?” Akajibu: “Hapana.” ´Amr akasema: “Je, unaona kuwa yule ambaye Allaah amemuahidi adhabu kwa tendo fulani atavunja ahadi hiyo?” Abu ´Amr akajibu: “Ee Abu ´Uthmaan! Umeingia ndani ya kosa hilo kwa sababu si mwarabu.  Ahadi ni tofauti na tishio. Waarabu hawaoni kuwa ni fedheha wala kuvunja ahadi ikiwa mtu ikiwa atatishia kisha asitekeleze. Bali wanaona hilo kuwa ni ukarimu na tabia njema. Lakini kuvunja ahadi ni kwamba uahidi jambo zuri kisha usilifanye.”

17 – Mu´aadh bin Mu´aadh amesema:

”Nilimuuliza ´Amr bin ´Ubayd anasemaje juu ya Hadiyth ya al-Hasan kwamba ´Uthmaan alimwacha mke wa Rahmaan bin ´Awf kurithi baada ya kumalizika muda wa eda?” Akajibu: ”Uthmaan hakuwa ni Sunnah yoyote.'”

18 – ´Abdullaah bin Salamah al-Hadhwramiy amesema:

“Nilimsikia ´Amr bin ´Ubayd akisema: ”Nimemsikia ´Aliy, ´Uthmaan, Twalhah na az-Zubayr wangeshuhudia mbele yangu kuhusu kamba ya kiatu basi nisingekubali ushahidi wao.'”

19 – Yahyaa amesema:

“Nimemsikia Yahyaa akisema: ”Nilimuuliza ´Amr bin ´Ubayd ninianachosema kuhusu Hadiyth ya al-Hasan kutoka kwa Samurah (Radhiya Allaahu ´anh) kuhusu kupumzika kidogo mara mbili katika swalah (baada ya Takbiyrat-ul-Ihraam na baada ya kusoma Suura kabla ya Rukuu´)?” ´Amr akasema: ”Unataka nini kutoka kwa Samurah? Allaah amlaani Samurah.'”

20 – ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz amesema:

“Ee Ghaylaan! Nimepata khabari kwamba unazungumza kuhusu makadirio.” Ghaylaan akasema: “Wananisemea uwongo, ee kiongozi wa waumini.” ´Umar akasema: “Nisomee Suurah Yaa Siyn.” Akasoma:

يس وَالْقُرْآنِ الْحَكِيمِ إِنَّكَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ تَنزِيلَ الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أُنذِرَ آبَاؤُهُمْ فَهُمْ غَافِلُونَ لَقَدْ حَقَّ الْقَوْلُ عَلَىٰ أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ إِنَّا جَعَلْنَا فِي أَعْنَاقِهِمْ أَغْلَالًا فَهِيَ إِلَى الْأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ وَجَعَلْنَا مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَاهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ

”Yaa Siyn. Naapa kwa Qur-aan yenye hekima. Hakika wewe bila shaka ni miongoni mwa Mitume; uko juu ya Njia iliyonyooka. Ni Uteremsho wa Mwenye nguvu Aliyeshinda, Mwenye kurehemu; ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao ni wenye kughafilika. Kwa hakika imethibiti kauli [ya adhabu] juu ya wengi wao, kwa hiyo hawaamini. Hakika Sisi tumeweka kwenye shingo zao minyororo ikawafika videvuni, basi vichwa vyao vinanyanyuka juu na kufumba macho. Tumeweka mbele yao kizuizi na nyuma yao kizuizi, Tukawafunika, basi wao hawaoni.”[1]

Ghaylaan akasema: “Ee kiongozi wa waumini! Ni kama kwamba sia sijawahi kuisoma isipokuwa leo. Ee kiongozi wa waumini! Nakushuhudisha ya kwamba najirejea maoni yangu juu ya makadirio.” ´Umar akasema: “Ee Allaah! Akiwa ni mkweli, basi ikubali tawbah yake na ikiwa ni mwongo, basi mfanye kuwa ishara kwa waumini.”

Ibrahim alitusimulia: Abu Musa aliniambia: Durrast bin Ziyad Abu Al-Hasan alikuwa akisema kuhusu Bani Qais bin Aqata kutoka kwa Muhammad bin Amru bin Alqama, akasema: Al-Zuhri alinisimulia: Umar bin Abdulaziz alikuwa ameketi, na Ghaylan alikuwa mbele yake. Umar akasema: “Ewe Ghaylan, ni jambo gani hili jipya umeleta katika Uislamu?”

21 – az-Zuhriy amesema:

”Niliingia kwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz na nikamuona Ghaylaan ameketi mbele yake. Akasema: “Ee Ghaylaan! Nini hiki? Umezusha katika Uislamu?” Akasema: “Sijazusha chochote ndani ya Uislamu, ee kiongozi wa waumini.” Akasema: “Ndiyo, maoni yako kuhusu makadirio. Unaweza kusoma Yaa Siyn?” Akasema: ”Ndio.” Akaanza kusoma hadi alipofika kwenye:

إِنَّا جَعَلْنَا فِي أَعْنَاقِهِمْ أَغْلَالًا

”Hakika Sisi tumeweka kwenye shingo zao minyororo… ”

Ndipo ´Umar akasema: ”Simama hapo.” Ni nani aliyeweka shingoni mwao minyororo?” Akasema: ”Naapa kwa Allaah kwamba sijui.” ´Umar akasema: ”Naapa kwa Allaah ni Allaah. Soma:

وَجَعَلْنَا مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا

”… Tumeweka mbele yao kizuizi na nyuma yao kizuizi…”

Ni kina nani waliowekewa mbele yao na nyuma yao kizuizi?” Ghaylaan akasema: “Naapa kwa Allaah kwamba sijui.” ´Umar akasema: ”Naapa kwa Allaah ni Allaah.” Ghaylaan akasema: ”Sikujua kuwa ni hivo, ee kiongozi wa waumini. Namuomba Allaah msamaha na ninatubu Kwake.” ´Umar akasema: ”Ee Allaah! Akiwa ni mkweli basi ikubali tawbah yake. Na akiwa ni mwongo, basi usimfishe mpaka umwonjeshe uchungu wa upanga.” ´Umar akafariki na akamwachia uongozi Yaziyd. Yaziyd akafariki  na akamuachia uongozi Hishaam bin ´Abdil-Malik. Nilipoingia kwake, nikamuona Ghaylaan amekaa mbele yake. Akasema: “Nyosha mikono yako.”
Akainyoosha mikono yake na akaikata kwa upanga. Kisha akasema: ”Nyoosha mguu wako.” Akaunyoosha na akaukata kwa upanga. Kisha akamsulubu. Nikakumbuka du´aa ya ´Umar – Allaah awe radhi naye.”

Mwisho wa kitabu na himdi njema zote ni stahiki ya Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na amani ziwe juu ya Bwana wetu Muhammad na jamaa zake.

[1] 36:1-9

  • Muhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy (afk. 385)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Akhbaar ´Amr bin ´Ubayd bin Baab al-Mu´taziliy, uk. 100-109
  • Imechapishwa: 22/11/2025