Nimeulizwa juu ya hali ya Yemen na kama kujiunga na maaskari wa nchi dhidi ya Huuthiyyah ni Jihaad.

Kuwapiga vita Huuthiyyah pamoja na nchi na chini ya uangalizi wake ni katika Jihaad kwa lengo la kujihami. Kuwapiga vita Raafidhwah hawa makafiri ni wajibu kwa kila ambaye ana jukumu kwa matendo yake na ana uwezo wa kuchangia kwa kuingia mwenyewe, mwenyewe na mali yake au mali yake tu. Hili ni kutokamana na sababu mbili:

1- Huuthiyyah sio kundi la waasi; bali ni kundi la kikafiri, waritadi na Raafidhwah. Wanapata sapoti na nchi ya Iran ya ki-Raafidhwah. Huyu mshambulizi kafiri lengo lake sio kutaka kupata uongozi peke yake. Lengo lake ni kutaka kuutokomeza Uislamu na Sunnah. Fahamuni, enyi waislamu na Ahl-us-Sunnah mlioko Yemen ilio ghali!

2- Kiongozi wa Kishari´ah ´Abdu Rabbin bin Mansuur bin Haadiy amewaamrisha watu kutoka na kupigana. Wakati mtawala anapotoa amri juu ya vita inakuwa ni wajibu kwa watu wote kama tulivyotangulia kusema. Yule mwenye kuacha kutii amri yake na kuwapiga vita makafiri hawa Raafidhwah Baatwiniyyah au akamili kwao ni mpiganaji mhalifu na mueneza ufisadi katika ardhi na ni mwenye kumuasi Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ee Ahl-us-Sunnah! Pambaneni pasi na kujali lawama za wenye kulaumu. Jiandaeni, mtiini kiongozi wenu na jikurubisheni kwa Allaah kwa kuwapiga vita makafiri hawa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna Hijrah baada ya kutekwa [Makkah]. Mnapoamrishwa kutoka [vitani], tokeni [mwende vitani].”

Mmeamrishwa kutoka kwenda vitani. Kwa ajili hiyo ni wajibu kwenu kutii. Mtakeni Allaah msaada, msubiri na mtarajie malipo. Tambueni fika ya kwamba kuwapiga vita makafiri hawa Raafidhwah Baatwiniyyah ni Jihaad kwa lengo la kujihami; kuitetea dini, heshima, akili, nafsi na mali. Mcheni Allaah juu ya dini yenu. [Sauti haiko wazi] na tarajieni malipo kutoka kwa Allaah.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=151367 Tarehe: 1436-06-05/2015-03-25
  • Imechapishwa: 20/09/2020