Kuwadhihaki wenye ndevu na wenye kufupisha nguo zao

Swali: Ni ipi hukumu ya kudhihaki ndevu na kufupisha nguo juu ya vifundo vya miguu?

Jibu: Hili ni jambo haramu. Kudhihaki ndevu na kudhihaki kufupisha nguo isiyoshuke chini ya kongo mbili za miguu ni maovu makubwa. Huenda mwenye kufanya hivyo akawa mwenye kuritadi. Huenda akakufuru kwa jambo hilo. Ikiwa lengo lake ni kudhihaki dini, basi kunaweza kuwa kuritadi kutoka katika Uislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?”  Msitoe udhuru; mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.”[1]

Kwa hiyo kuzichezea sherehe ndevu, swalah, swawm, kufupisha nguo na kutoivaa chini ya kongo mbili za miguu ni khatari kubwa. Ikiwa lengo lake ni kudharau dini na kuitia mapungufu, basi huko ni kuritadi kutoka katika Uislamu.

[1] 09:65-66

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30104/ما-حكم-الاستهزاء-باللحية-وتقصير-الثياب
  • Imechapishwa: 11/09/2025