Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa ´Aaishah 05

93 – Abu ´Ubaydillaah al-Qaasim bin Ismaa´iyl ametuhadithia: ´Abdullaah bin Abiy ´Abdillaah ash-Shaybaaniy ametuhadithia: Muhammad bin ´Ubaadah ametuhadithia: Haatim bin Ismaa´iyl ametuhadithia, kutoka kwa Mudhwar bin Kathiyr, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa Sa´iyd, kutoka kwa ´Urwah, kutoka kwa ´Aaishah ambaye kasema:

“Usiku wa nusu Sha´baan Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kwenye blanketi yangu. Naapa kwa Allaah! Haikuwa ya hariri, misitarimisitari pamba wala.”Tukasema: “Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu! Ilikuwa ya nini?” Akasema: “Kitambara chake kilikuwa cha manyoya na kwa ndani yake kilikuwa cha manyoya ya ngamia. Nilihisi pengine amewaendea baadhi ya wakeze.”

Kisha akataja mfano wake.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 172
  • Imechapishwa: 13/01/2021