96- Yazaadaad bin ´Abdir-Rahmaan al-Kaatib ametuhadithia: Abu Sa´iyd al-Ashajj ametuhadithia: ´Uqbah bin Khaalid ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Umm Salamah aliyesema:

“Uzuri ulioje wa siku ambayo Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini ya dunia. Wakasema: “Ni siku gani hiyo, ee mama wa waumini?” Akasema: “Ni siku ya ´Arafah.”[1]

Mwisho

Himdi zote njema anastahiki Allaah pekee. Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad na kizazi chake.

[1] Cheni ya wapokezi ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 175
  • Imechapishwa: 14/01/2021