Swali: Je, kufanya ndoa Sha´abaan na baada ya ´Aswr ni katika Sunnah?

Jibu: Ndoa Sha´abaan ni mubaha , hakuna fadhila maalum. Fadhilah zimekuja kuoa baina ya ´iyd mbili, Mtume (´alayhis-Salaam) alimuoa ´Aaishah au kwa maana hii baina ya ´iyd mbili. Kadiri utavyoweza, ni mamoja ikiwa ni Shawwal au Dhul-Qa’dah. Ama mbali na hiyo miezi ni mubaha isipokuwa tu wakati wa Ihraam. Ikiwa wewe ni Muhrim , sawa ikiwa ni Hajj au ´Umrah haijuzu kufanya ndoa. Wala haijuzu kuchumbia wala kuchumbiwa, kwa kuwa ni Muhrim. Lakini kwa mtu ambae si Muhrim wakati wowote anaweza kuoa au kuolewa.

Swali: Kuoa baada ya ´Aswr?

Jibu: Hakuna kitu. Wakati wowote sawa usiku au mchana mtu anaweza kufanya ndoa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=2457
  • Imechapishwa: 22/09/2020