Swali: Inajuzu kwangu kumwangalia mwanamke ambaye nataka kumuoa bila ya familia yake kujua? Kwa mfano amehudhuria kwa ndugu zangu nikamwangalia bila ya yeye na familia yake kujua kwa vile – kwa idhini ya Allaah – nina azma ya kumposa lakini hata hivyo bado sijamtolea mahari. Kilichopitika tu ni kuwa yeye na wazazi wake wameafiki kabla ya mimi mwenyewe binafsi kwenda kujitambulisha. Nimeswali swalah ya Istikhaarah. Je, kuangalia kwangu huku kunajuzu?
Jibu: Kuangalia kwako huku kunajuzu[1]. Mtu akiwa na azma ya kumuoa na mwaname na akawa na dhana yenye nguvu kuwa atakubaliwa, inafaa kwake kumtazama. Bali imesuniwa kwake kumtazama. Kwa sharti wasikae faragha na ajiamini kutotokea fitina. Ikiwa hatokuwa kukaa faragha na akaamini kutotokea fitina na akamwangalia yale yenye kutosha ambayo yanamvutia – kama kuangalia uso, kichwa, vitanga vya mikono na miguu – ni sawa. Bali ni katika mambo yaliyowekwa katika Shari´ah. Mambo haya ni salama zaidi kwa kuwadumisha wanandoa na kuwaunganisha.
Kuna watu wanauliza kama inajuzu kumuomba picha yake? Haijuzu.
Mosi: Picha inaweza kubaki mikononi mwa huyo mposaji hata kama atakataliwa.
Pili: Picha haiwakilishi uhalisia wa kweli. Picha aidha inaweza kumfanya kuonekana mbaya kama ambavyo vilevile inaweza kumfanya kuonekana mzuri. Matokeo yake mtu akadanganyika.
Tatu: Haifai kwa mtu kumwacha mwanaume akaangalia picha ya ahli zake; wasichana wake, dada zake na mfano wa hao. Bali hata kwake – yaani huyo mposaji – haijuzu kuiangalia kutokana na fitina inayopatikana kwa kufanya hivo na huenda vilevile picha hii ikaanguka mikononi mwa watu waovu na wakawaonyesha watu msichana wako. Hatimae msichana huyo akiwa mzuri inakuja kuwa ni fitina kwa watu. Na akiwa ni mbaya anakuja kusemwa vibaya.
[1] Tazama https://firqatunnajia.com/9-kumtazama-mwanamke-kwa-kujiiba-katika-mnasaba-wa-posa/
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (22)
- Imechapishwa: 30/12/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
9. Kumtazama mwanamke kwa kujiiba katika mnasaba wa posa
Inafaa kwake [mwanaume] kumwangalia [mwanamke] kwa kujiiba pasina yeye kujua. Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: "Nilimchumbia mwanamke. Nilikuwa nikijificha ili niangalie yale yatayonivutia kuweza kumuoa. Hivyo nikawa nimemuoa."[1] Muhammad bin Maslamah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: "Nilimchumbia mwanamke. Nilipanda juu ya mti wa mtende na kujificha ili niweze kumtazama."[2] Wakati walipomuuliza…
In "Haqq-uz-Zawjayn"
Mwanaume kumtazama mposwaji na kinyume chake
Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Mmoja wenu akimposa mwanamke, akiweza kumwangalia yale yatayomvutia kumuoa, basi na afanye hivo.”[1] Ni yepi ambayo inafaa kwa mposaji kuyatazama kwa mposwaji? Jibu: Atazame uso wake na mikono yake. Hayo ndio ambayo yanafaa kwake. Swali: Je, mwanamke anayo haki ya kuomba kumtazama…
In "Uchumba na uposaji"

Ni wajibu kumtazama mwanamke kabla ya kumuoa? Kunatazamwa nini?
https://www.youtube.com/watch?v=pXK02h6-YtI Swali: Kijana anapotaka kumposa mmoja katika wasichana. Katika hali hii, je ni wajibu kwake (kijana huyo) kumuona? Na je, ni sawa msichana huyo kufunua kichwa chake ili abainishe uzuri wake zaidi kwa mposaji wake? Jibu: Hakuna ubaya, lakini sio wajibu bali ni jambo limependekezwa. Ni jambo limependekezwa (kijana huyo)…
In "Uchumba na uposaji"