Swali: Je, inajuzu kumsusa mtu asiyeswali katu hata kama atakuwa ni kaka yangu?

Jibu: Ndio. Yule ambaye anakusudia kuacha swalah, huyu sio muislamu:

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ

“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kwamba wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao.” (58:22)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15082
  • Imechapishwa: 20/09/2020