Swali: Ni ipi hukumu ya kuashiria mkono ndani ya swalah wakati mtu anapotoa salamu na kumaliza swalah ambapo anageuza mikono na kusema:

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yenu.”

 upande wa kulia:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”

upande wa kushoto?

Jibu: Sunnah katika Tasliym mswaliji anatakiwa kusema:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”

upande wa kuliani mwake.

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”

upande wa kushotoni mwake. Asiashirie kwa mikono yake. Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir bin Samurah ambaye amesema: “Niliswali pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na tulikuwa tunapotoa salamu tunaashiria kwa mikono yetu:

السلام عليكم السلام عليكم

“Amani ya Allaah iwe juu yenu. Amani ya Allaah iwe juu yenu.”

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatutazama na akasema:

“Ni kwa nini mnaashiria kwa mikono yetu kana kwamba ni mikia ya farasi ilio na wasiwasi? Anapoleta Tasliym mmoja wenu basi ageukie upande wa mwenzake na wala asiashirie kwa mkono wake.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz Aalus-Shaykh

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (05/409) nr. (15441)
  • Imechapishwa: 13/05/2022