Kitabu cha kipekee ambacho ni miujiza

Haafidhw as-Sulaymaan amesema:

“Muhammad bin Naswr al-Marwaziy ni imamu wa maimamu, zawadi tumepewa kutoka mbinguni. Alikuwa anaishi Samarkanda na alimsikia Yahyaa bin Yahyaa, ´Abdaan, ´Abdullaah al-Musnaadiy na Ishaaq. Ametunga kitabu “Ta´dhwiym Qadr-is-Swalaah”, Raf´-ul-Yadayn” na vitabu vyengine vya kimiujiza.”

Hivo ndivo anavosema as-Sulaymaan, lakini Qur-aan pekee ndio miujiza. Kisha akasema:

“Yeye na Swalaah Jazarah walifariki mwaka wa 294.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/37)
  • Imechapishwa: 20/11/2020