Josho la lazima mara moja kwa wiki

Swali: Je, ni lazima kwa wanaume na wanawake kuoga wasipohudhuria katika swalah ya ijumaa?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Josho la siku ya ijumaa ni wajibu kwa kila mwenye kuota.”[1]

Kinachodhihiri ni kwamba josho hilo ni kwa ajili ya siku ya ijumaa. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayekuja ijumaa basi aoge.”[2]

Hadiyth hii pia inafahamisha juu ya ulazima wa kuoga siku ya ijumaa. Hadiyth nyingine inasema:

“Ni haki kwa kila muislamu kuoga mara moja kwa wiki; aoshe kichwa chake na mwili wake.”[3]

Kwa mujibu wa Hadiyth hii inajulisha kuwa mtu analazimika kuoga hata kama hakwenda kuswali swalah ya ijumaa. Hata hivyo sio lazima afanye hivo siku ya ijumaa midhali hakwenda, anaweza kuoga siku nyingine yoyote. Muislamu anapaswa kuoga mara moja kwa wiki.

Kuhusu Hadiyth inayosema:

“Yule asiyekuja katika ijumaa, basi hakuna josho juu yake.”

udhahiri ni kwamba sio Swahiyh. Aidha maneno yake ´Abdullaah bin ´Umar sio hoja.

[1] Muslim.

[2] Ibn Maajah. Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (707).

[3] al-Bukhaariy (896) na Muslim (855).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 368-369
  • Imechapishwa: 01/07/2025