Je, mume naye analaaniwa kwa kukataa kumpa mke?

Swali: Mwanamke akimwita mume wake kwenye kitanda ni wajibu kwake [mume] kumuitikia kama jinsi hali ilivyo kinyume chake? Je, maneno Yake (Ta´ala):

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Na hao wanawake wana kama ile haki iliyo juu yao kwa mujibu wa Shari´ah.” (02:228)

Inasihi kuwa dalili katika masuala haya?

Jibu: Masuala ni kwamba, mume akimwita mke wake kwenye kitanda na akakataa, Malaika wanamlaani. Ama ikiwa na yeye akimuomba mume, ana haki ilio na mipaka. Imepokelewa kutoka kwa Salaf ya kwamba mume anaweza kuwa mbali na mke wake – yaani hamwingilii – kwa muda wa miezi minne. Baada ya hapo [mke] ana haki ya kuomba [haki yake]. Mume anaweza kuwa sio muweza, anaweza kuwa amesibiwa na mambo na akawa sio muweza wa kumtimizia haja zake. Hazingatiwi kuwa ni mwenye kupata madhambi. Na ni juu yake ikiwa ana uwezo amtimizie haja zake mwanamke. Hii ni Sunnah ya Allaah kwa viumbe Wake, ya kwamba mwanamke anamuhitajia mume na mume anamuhitajia mwanamke.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.njza.net/Default_ar.aspx?ID=98
  • Imechapishwa: 22/09/2020