Inajuzu kwa mwanamke kuwaswalisha wanawake wenzake nyumbani kwa maiti?

Inajuzu kwa mwanamke kuwaswalisha wanawake wenzake nyumbani kwa maiti?

Swali: Inajuzu kwa mwanamke kuwakusanya wanawake ambao ni ndugu wa maiti na akawaswalisha swalah ya jeneza kumswalia maiti wao ndani ya nyumba hiyo?

Jibu: Ndio. Ni sawa kwa mwanamke kuswali swalah ya jeneza. Ni mamoja akamswalia msikitini pamoja na wengine au akamswalia nyumbani kwa maiti huyo. Kwa kuwa wanawake hawakukatazwa kumswalia maiti. Walichokatazwa ni kuyatembelea makaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi, wale wenye kufanya ni mahali pa kuswalia na wale wenye kuyawekea mataa[1]. Hapa inahusiana na pale atapokusudia kuyatembelea. Upande mwingine ikiwa hakukusudia kuyatembelea, kwa mfano ameenda katika shughuli zake na akawa ameyapitia makaburi, ni sawa akasimama na akawatolea Salaam waliyomo ndani ya makaburi na akawaombea du´aa.

[1] Ahmad (01/229), Abu uDaawuud (3236), at-Tirmidhiy (320) aliyeifanya Hadiyth hiyo kuwa ni nzuri (Hasan), an-Nasaa´iy (2045).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/157-158)
  • Imechapishwa: 15/09/2021